Dodoma FM

Mtindo wa maisha chanzo cha msongo wa mawazo kwa wanafunzi vyuoni

12 December 2025, 16:09

Ni vyema kila kijana akajua lengo lililompeleka chuo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.Picha na Mtandao.

Taswira ya Habari imetembelea baadhi ya vyuo vilivyopo jijini Dodoma nakuzungumza na wanafunzi ambapo wamesema.

Na Bennard Filbert.
Wanafunzi wa vyuo nchini imetajwa kuwa chanzo kikuu cha msongo wa Mawazo hali inayopelekea baadhi yao kuchukua maamuzi ya kujiua.

Hayo yanajiri kutokana na wimbi la baadhi ya vijana wanaosoma vyuo vikuu nchini kukatisha uhai wao kwa sababu mbalimbali.

Muhibu Mtahu ni mtaalamu wa saikolojia ameiambia taswira ya Habari kuwa vijana wengi waliopo vyuoni wanajikuta kwenye sintofahamu baada ya kujihusisha na vitu ambavyo baadae vina garimu maisha yao.
Amesema ni vyema kila kijana akajua lengo lililompeleka chuo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kipindi cha baadae.

Sauti ya Muhibu Mtahu.

Taswira ya Habari imetembelea baadhi ya vyuo vilivyopo jijini Dodoma nakuzungumza na wanafunzi ambapo wamesema.

Sauti za wanafunzi.

Kujiua ni moja ya sababu kuu za vifo kwa watu wenye umri wa miaka 15–29, ambao ni umri unaofanana na wanafunzi wengi wa chuo Utafiti uliofanywa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa vyuo ulionyesha kuwa 38% ya wanafunzi walikuwa na msongo mkali wa mawazo,46.5% walikuwa na kiwango cha wastani huku 15.5% walikuwa na msongo mdogo.