

30 April 2025, 5:36 pm
Taswira ya habari imezungumza na mashuhuda pamoja na mwenyekiti wa kijiji hicho juu ya tukio hilo.
Na Kitana Hamis.
Kijana mmoja aliye Famika kwajina la Mohamed Khamisi mwenye umri wa Miaka 22 Mkazi wa Ndirigishi Wilayani Kiteto Mkoani Manyara amemuuwa Baba yake Mzazi na kumkata sehemu zake za siri.
Sababu za kijana huyo kufanya tukio hilo bado hazijajulikana na japo watu wa karibu wanadai kijana huyo alikuwa na mgogoro wa mara kwa mara na baba yake.