Dodoma FM

Mambo ya kuzingatia kuepuka kipindupindu

17 January 2024, 8:50 am

Picha ni Afisa Afya Mkoa wa Dodoma Nelson Rumbeli akitoa elimu kuhusu ugonjwa wa kipindupindu. Picha na Yussuph Hassan.

Jamii imekumbushwa kuendelea kunawa na maji tiririka pindi wanapotoka maliwato ili kujilinda na kujikinga na maradhi hayo.

Na Yussuph Hassan.
Ikiwa tunaendelea kuelimisha Jamii kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu, Jamii imesisitizwa kuhakikisha wanajenga na kutumia Vyoo bora ili kupekuna na ugonjwa wa kipindupindu.
Pia imekumbushwa kuendelea kunawa na maji tiririka pindi wanapotoka maliwato ili kujilinda na kujikinga na maradhi hayo
Hayo yamesemwa na Afisa Afya Mkoa wa Dodoma Nelson Rumbeli wakati akizungumza na Dodoma Tv kuhusu umuhimu wa Jamii kujikinga na ugonjwa kipindupindu