Dodoma FM

CVT kutoa vipimo bure siku ya uono Duniani

12 October 2022, 11:30 am

Na; Alfred Bulahya

Kuelekea siku ya Uono Duniani octoba 13, Clinic ya Macho ya CVT iliyopo Jijini Dodoma imepanga kutoa huduma za upimaji wa macho bure katika siku hiyo na kutoa huduma ya upasuaji na miwani kwa gharama nafuu ili kuisaidia jamii kutambua hali ya afya ya macho kwa ujumla .

Hayo yamebainishwa na Meneja wa clinic hiyo Lulu Molel wakati akizungumza na Taswira ya habari ofisin kwake ambapo amesema Lengo la kufanya hivyo ni kutaka jamii itambue hali ya afya zao na kuchukua hatua kwa wale wanaobainika kuwa na  changamoto.

.

Amesema wamepanga kuwaona watu zaidi ya 100 kwa siku hiyo huku akiwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwani ni muhimu kutambua afya zao ili kuchukua hatua za haraka.

Daktari bingwa wa macho kutoka katika clinic hiyo Dkt Nelson Mtajwaa amesema kwa sasa wamekuwa wakipokea wagonjwa wengi wenye tatizo na mtoto wa jicho na uoni hafifu hasa mbali huku akitaja sababu za kuwepo kwa wagonjwa wengi wa matatizo hayo.

.

Naye Afisa mteknolojia Macho bw Charles Ngowi  amelitaja kundi la watoto kuanzia miaka 7 hadi 18 kuwa limekuwa likipata tatizo la uoni hafifu hasa wa mbali kwa kiwango kikubwa kutokana na kutumia vitu vyenye mwanga mkali kwa muda mrefu huku akiwataka kuachana na dhana potofu kuwa mtu akitumia miwani anaongeza tatizo la uoni hafifu.

.

Oktoba 13 kila mwaka ni siku ya uono duniani ambapo kwa kwaka huu siku hiyo itaadhimisha ikiwa na kaulimbiu isemayo Penda Macho yako