Dodoma FM

TASAF yazidi kunufaisha kaya masikini

5 February 2021, 4:40 pm

Na,Mindi Joseph,

Dodoma.

Kaya milion moja na laki mbili zinatarajiwa kushiriki katika miradi ya kuinua uchumi wa kaya kati ya kaya milion 1 laki nne na nusu zilizopo katika kipindi cha pili cha awamu ya 3, ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF.
Akizungumza leo jijini Dodoma baada ya kutembelea kaya ambazo ni wanufaika wa mpango wa Tasaf Mkurungezi wa Programu za jamii TASAF Amadeus Kamagenge, amaesema katika kuinua uchumi wa kaya vikundi elfu 23 vimeundwa na wanufaika hao na wameweka akiba zaidi ya bilioni 5.
Ameongeza kuwa serikali imewekeza fedha Trilion 2.3 kuinua kaya masikini na kaya za walengwa ambao wanafanya kazi wataingizwa katika program ambayo itatekelezwa kila Kijiji kipindi cha pili awamu ya 3 , ambapo zaidi ya miradi elfu 30 inatarajiwa kutekelezwa.

Kwa upande wake Bogit Samhenda mratibu wa TASAF Mkoa wa Dodoma amesema kuwa Mkoa huo uliingia katika program hiyo mwaka 2014 na Vijiji 386 kati 582 katika mkoa wa dodoma wamenufaika na mfuko huo.

Naye mnufaika wa TASAF Bi.Winifrida Hosea kutoka Mtaa wa Mwaja jijini Dodoma amewataka watazania wengine wanaopata fedha hizo kuwekeza katika miradi itakayowasiadia kujikwamua kiuchumi.