Dodoma FM

Bei ya maharage yazidi kupaa sokoni

17 August 2023, 4:19 pm

Bei ya maharage imeanza kupanda tena baada ya siku chache kushuka hali inayowaathiri wananchi. Picha na Mariam Msagati.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ilibainisha bei ya mazao ya chakula ikiwemo maharage imepungua kutoka asilimia 33.5 hadi asilimia 28.3 kwa mwaka ulioshia mwezi Julai 2023 ikilinganishwa na mwaka ulioshia mwezi Juni 2023.

Na Mariam Msagati.

Bei ya maharage imeendelea kupanda katika masoko mbalimbali Jijini Dodoma ikiwemo soko la Majengo pamoja na Sabasaba huku sababu kubwa ikiwa ni uhaba wa bidhaa hiyo kutoka kwa wakulima.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wafanyabiashara wa bidhaa hiyo ambapo wanasema kuwa licha ya bidhaa hiyo kushuka kwa siku za hivi karibuni lakini kwa sasa bei ya bidhaa hiyo imepanda ghafla.

Sauti za wafanyabiashara.
Mfanyabiashara wa maharage katika soko la Majengo jijini Dodoma akiongea na Dodoma Tv. Picha na Mariam Msagati.

Baadhi ya wananchi pamoja na wafanyabiashara wa chakula wanasema kuwa kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo kunaendelea kuwaathiri hususani katika suala la kupata wateja.

Sauti za baadhi ya Wanunuzi.