Dodoma FM

Mgogoro wa vitongoji viwili wakwamisha ujenzi wa Zahanati Songolo

15 March 2024, 7:03 pm

Picha ni Mkazi wa kijiji cha Madaha akieleza adha wanazo zipata hasawnapofuata huduma ya Afya mbali . Picha na Mindi Joseph.

Vitongoji hivi vilipinga ujenzi wa zahanati hiyo na kususa kushiriki hali iliyochangia Wananchi wa kijiji cha Madaha kutembea zaidi ya kilomita 20 kufuata huduma za afya katika Kituo cha afya Hamai.

Na Mindi Joseph.
Uwepo wa Mgogoro baina ya vitogoji vya madaha kati na Podolia katika kijiji cha Madaha Kata ya Songolo wilayani Chemba umechangia kukwamisha zoezi la ujenzi wa zahanati.

Nimezungumza na Mwenyekiti wa kijiji cha madaha Fadhili Swalehe kwa njia ya Simu anasema ujenzi wa zahanati hiyo una mwaka mmoja tangu umekwama.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha madaha Fadhili Swalehe.
Picha ni Diwani wa kata ya Songolo Mohamed Mayingu .Picha Mindi Joseph.

Wananchi wa kijiji hicho nao walikuwa na hiki cha kusema.

Sauti za Wananchi wa kijiji hicho .

Diwani wa kata ya Songolo Mohamed Mayingu anasema jitihada zinaendelea kufanyika ili kuwashawishi wananchi.

Sauti ya Diwani wa kata ya Songolo Mohamed Mayingu .