Dodoma FM
Dodoma FM
15 April 2026, 5:40 pm

Taswira ya habari imezingumza na Mwenyekiti wa Kijiji cha Muungano Bw. Matonya Mtukamsihi ambaye amekiri kusikia Malalamiko hayo kutoka Kwa wananchi.
Na Victor Chigwada.
Baadhi ya wanawake katika kijiji cha Muungano wilayani Chamwino wamelalamikia kuuziwa kadi wanapo wapeleka watoto kuanza clinic.
Kwa mujibu wa sera ya Afya inazielekeza Zahanati na vituo vyote vya afya nchini kutoa vitabu vya kliniki bure kwa watoto chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito.
Serikali imeendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kote nchini lakini licha ya maboresho hayo kufanyika sehemu mbalimbali hapa nchini lakini bado baadhi ya wananchi bado wanalalamika kulipia gharama za matibabu kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano.
Taswira ya habari imezingumza na Mwenyekiti wa Kijiji cha Muungano Bw. Matonya Mtukamsihi ambaye amekiri kusikia Malalamiko hayo kutoka Kwa wananchi na alipo fatilia alibaini gharama zinazo tozwa kwa ajili ya kadi hizo ni gharama kidogo zinazo tumika kuchapisha kadi hizo za clinik.
Aidha na wananchi wa Muungano wamesema kuwa kuchangia gharama za makadi na matibabu Kwa watoto ni jambo linalo washangaza ukilinganisha na maeneo mengine kwani haiwezekani zahanati ikose kadi za akinamama na watoto huku hospitali binafsi kadi hizo zikipatikana.