Dodoma FM

Jamii yatakiwa kujenga ushirikiano na tume ya haki za binadamu

9 April 2026, 13:08

Jamii nyingi zimekuwa zikipoteza haki zao kutokana na kutokuwa na uelewa ,Picha na Tume ya maadili.

Tume ya Haki za Binadamu kwa mujibu wa Katiba ya nchi ibara ya 129 mpaka ibaraya 131 imeainisha majukumu kwa ujumla na namna ambavyo utekelezwaji wake ulivyo na kupitia utekelezwaji huo jamii hupata maendeleo kwa kushirikiana na viongozi pasipo kuvunja haki.

Na Jerome John.

Jamii imetakiwa kushirikiana na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutoa taarifa pindi uvunjifu wa haki zozote  za binadamu unapo tokea.

Akizungumza mapema leo naTaswiraya Habari mchunguzi mkuu msaidizi Halfan Mbotea kutoka Tume hiyo amesema kumekuwepo na viashiria  au matukio ya uvunjifu wa haki  za binadamu nchini hivyo tume hiyo imekuwa ikifanya uchunguzi na kuhakikisha hatua mbalimbali zinachukuliwa na wahusika kuwajibishwa.

Aidha afisa huyo amebainisha kuwa kutokana na baadhi ya wanajamii kutokuwa na uelewa wa haki zao wamekuwa wakipoteza haki na wakati mwingine kutendewa ndivyosivyo na kushindwa kutoa taarifa katika tume hiyo.

Sauti ya Halfan Mbotea .