Dodoma FM

Wananchi watakiwa kupima afya kubaini magonjwa yasiyoambukiza

10 November 2026, 16:26

Picha ni mwananchi na mtoa huduma katika kitu cha afya akifanya vipimo kwa mgonjwa. Picha na Mwananchi.

Katika kuadhimisha Wiki ya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza, wananchi wametakiwa kuondoa hofu na kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kubaini magonjwa hayo mapema, hata pale wanapokuwa hawana dalili zozote.

Na Daniel Njau.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Misanga, ambaye amesema baadhi ya magonjwa hayo yanaweza kumpata mtu bila kuonesha dalili, hivyo uchunguzi wa afya katika vituo vya kutolea huduma ni muhimu katika kuyabaini na kuchukua hatua za mapema.

Kwa upande wake, Afisa Uuguzi Nafukwe Omari amesema huduma za uchunguzi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza zinatolewa bure bila malipo yoyote, kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa moja na nusu asubuhi.

Amehimiza wananchi kutumia fursa hiyo kujitokeza kwa wingi kupima afya zao, akieleza kuwa uchunguzi wa mapema ni hatua muhimu katika kujikinga na madhara yanayoweza kusababishwa na magonjwa hayo.

Sauti ya Mratibu wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Misanga