Wito watolewa jamii kulinda haki, ustawi wa wazee
15 October 2026, 16:29

Jamii imetakuwa kutambua umuhimu wa familia na jamii kushirikiana katika kuwahudumia wazee ili kuhakikisha wanaishi katika mazingira yenye upendo, heshima na usalama. huku wakitakiwa kutipoti hali na tabia zisizo faa zinazopelekea wazee kukosa haki zao kutokomezwa kisheria.
Na Leokadia Andrew
Serikali na jamii zimetakiwa kuimarisha juhudi za kulinda haki za wazee kwa kuhakikisha wanapata huduma bora za afya, mahitaji muhimu na fursa ya kushiriki katika maamuzi yanayohusu maisha yao.
Wito huo umetolewa na Katibu wa Baraza la Ushauri la Wazee Manispaa ya Kahama, Andarson Lymo, aliyesema ni muhimu wazee kulindwa, kuheshimiwa na kuthaminiwa ili waweze kuishi maisha yenye heshima na ustawi.
Amesisitiza kuwa wazee wanapaswa kupata haki zao na huduma muhimu zinazowawezesha kuishi katika mazingira salama na yenye kuwajali.
Kwa upande wake, Mzee Jumanne Kasuku amewataka vijana kuwa na moyo wa kuwajali wazee na kuwasaidia katika mahitaji yao ya kila siku, yakiwemo chakula, huduma za afya na mahitaji mengine ya kijamii.