Dodoma FM

Wahitimu wa vyuo vikuu wageukia fursa ya bodaboda

27 October 2026, 17:01

Picha ni kijana aliye aliyetumia changamoto ya ajira kuwa fursa ya kujitafutia kupitia biashara ya uendeshaji ya bodaboda. Picha na mwananchi.

Fursa za kujiajiri zimeendelea kuwa njia muhimu kwa vijana wanaohitimu vyuo katika kukabiliana na changamoto ya ajira na kujenga maisha yao kiuchumi. Baadhi yao wameamua kutumia shughuli za bodaboda kama chanzo cha kipato, wakitambua kuwa mafanikio hayategemei pekee kupata ajira rasmi, bali pia uwezo wa kutumia fursa zilizopo katika jamii.

Na Daniel Njau.

Shughuli za usafirishaji wa abiria kwa pikipiki maarufu kama bodaboda zimekuwa miongoni mwa fursa zinazotumiwa na baadhi ya vijana wanao hitimu vyuo kujiajiri, kujipatia kipato na kujenga msingi wa maendeleo yao ya kiuchumi.

Ahmed  Hasani, mkazi wa Dodoma na mhitimu wa shahada ya  kwanza ya ualimu, anasema alianza kufanya bodaboda akiwa mwanafunzi na sasa amefanikiwa kununua pikipiki nyingine kwaajili ya kuongeza kipato.Amesema mafanikio ya msomi yanahitaji uwezo wa kutambua na kutumia fursa zilizopo.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Waendesha Bodaboda na Bajaji Mkoa wa Dodoma (UMAPIDO), Remigius Fulgence, amesema vijana wengi hujiunga na sekta hiyo ili kujipatia kipato na kujikwamua kimaisha.

Hata hivyo, ameeleza kuwa baadhi ya waendesha bodaboda hukosa uelewa wa matumizi sahihi ya vyombo hivyo, hali inayoweza kusababisha ajali na matukio ya uhalifu. Aidha amesisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria na usalama barabarani.

Simulizi na Daniel Njau.