Dodoma FM

Shekimweri ataka mapungufu yarekebishwe Mayeto

4 January 2024, 4:28 pm

Picha ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma pamoja na Kaimu mkurugenzi na wadau mbalimbali wakiwa katika ziara hiyo.Picha na Halmashauri ya jiji la Dodoma.

Zoezi la ukaguzi wa shule mpya jijini Dodoma zinazo tarajia kufunguliwa january 8 umeendelea ambapo mkuu wa wilaya alipata wasaa wa kutembelea shule mbili ambazo pia zimekamilika.

Na Mariam Kasawa.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri ametaka mapungufu yaliyopo katika shule ya Msingi Mayeto kurekebishwa mara moja kabla ya Januari 8 mwaka huu.

Amesema hayo alipotembelea na kukagua shule hiyo mpya iliyopo Hombolo Makulu inayotarajia kufunguliwa hivi karibuni, Mkuu huyo wa wilaya amesema mapungufu yote kwenye shule hiyo yarekebishwe kabla ya jumatatu ambapo wanafunzi wanatarajia kuanza masomo.

Sauti ya Mh. Jabir Shekimweri.
Picha ni mmoja wa Wajumbe wa kamati ya ujenzi shuleni hapo akieleza changamoto ya maji ilivyo wakabili.Picha na Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Baadhi ya wazazi wakatoa mapendekezo yao na kueleza changamoto zilizopelekea vyoo vilivo jengwa shuleni hapo hadi sasa kukosa huduma ya maji.

Sauti ya Mzazi.

Nae Kaimu mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Mwl. Issa Kambi akaeleza mchakato uliopo wa kurekebisha baadhi ya mapungufu katika shule hiyo.

Sauti ya Mwl. Issa Kambi.