Dodoma FM

Rais Samia ashiriki kilele cha mbio za mwenge wa uhuru na kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha baba wa Taifa

14 October 2021, 12:37 pm

Na; Fred Cheti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani leo Oktoba 14 ameshiriki katika kilele cha mbio za mwenge wa uhuru pamoja na tukio la kumbikizi ya miaka 22 ya kifo cha baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza wakati akihutubia katika tukio hilo ililofanyika katika uwanja wa Magufuli wilayani Chato mkoani Geita Rais Samia amesema serikali imeamua kuunganisha shereha za kilele cha mbio za mwenge wa uhuru pamoja na kumbukizi ya kifo cha baba wa taifa , na wiki ya vijana ili kuwapa fursa watanzania wa kizazi cha leo na kijacho kukuza, kuenzi pamoja na kuendeleza shughuli za falsasa zinazongoza siasa nchini.

Aidha Mh. Rais amemuelezea Mwl. Nyerere kuwa alikuwa ni kuongoza wa pekee kuwahi kutokea katika bara la Afrika na duniani kwa kuwa alikuwa kiongozi jasiri,shupavu, mpenda haki na mwanamapinduzi hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kukumbuka na kuyaenzi yale yote mazuri aliyoturithisha.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi walioshiriki kuandaa matukio hayo Waziri wa Sera ,bunge,kazi ,ajira ,vijana na watu wenye ulemavu Mh. Jenista Mhagama amewashukuru wananchi pamoja na wadau wa maendeleo kwa kuendelea kuunga juhudi za serikali katika kujenga uchumi ambapo amesema kuwa jumla ya miradi 1067 yenye thamani ya shilingi trillioni 1.2 imezinduliwa na mingine kuwekewa mawe ya msingi katika mbio za mwenge mwaka huu.

Rais Samia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu leo amekuwa Mgeni rasmi katika kilele cha sherehe za mbio za uhuru zilizoambatana na kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere mkoani chato ambapo kauli mbiu katika sherehe hizo ni “Tehama ni Msingi wa Taifa Endelevu; Itumie kwa Usahihi na Uwajibikaji”