Dodoma FM

Kusajili alama ya bishara kumetajwa kuwa na umuhimu mkubwa

20 February 2023, 11:18 am

Kusajili alama ya bishara kumetajwa kuwa na umuhimu mkubwa katika kusaidia kuchangia ongezeko la wafanyabiashara.Picha na Martha Mgaya

Kusajili alama ya bishara kumetajwa kuwa na umuhimu mkubwa katika kusaidia kuchangia ongezeko la wafanyabiashara kujitangaza zaidi na kukuza biashara zao.

Na Thadei Tesha.

Hii ni kwa mujibu wa baadhi ya wafanyabiashara jijini dodoma ambapo wamesema upo umuhimu mkubwa kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa kusajili alama ya biashara kwani itawasaidia kutambulika zaidi na kujitangaza jambao ambalo liytasaidia kutanua zaidi biashara zao.

Wafanyabiashara jijini dodoma.

Brella ni moja ya taasisi inayohusika na usajili wa alama za biashara dodoma tv imetembelea ofisi za brella jijini dodoma kutaka kujua je ni upi umuhimu wa wafanyabiashara kuwa na alama ya biashara.

Brella.

Alama ya biashara au logo imekuwa na umuhimu mkubwa katika kuitambulisha jina la bidhaa pamoja na kampuni yake ambapo kwa mujibu wa wataalam mbalimbali wanasema kuwa upoo umuhimu mkubwa kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo.