Dodoma FM

Viongozi wa mitaa watakiwa kushirikiana na viongozi wa dini

16 October 2023, 6:24 pm

Picha ni wakazi wa vijiji vya Chiwe na Mtanana wakiwa katika mkutano huo. Picha na Seleman Kodima.

Pamoja na hayo, kanisa hilo linategemea kupitia ushirikiano waliongia na Foundation for Hope utaongeza  hali ya upatikanaji huduma za kiroho kwa ujenzi wa makanisa, sambamba na huduma za kijamii ikiwemo zahanati, uchimbaji wa visima vya maji na mahitaji mengine .

Na Seleman Kodima

Viongozi wa serikali za mitaa wametakiwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wa dini katika kuibua miradi ya maendeleo yenye lengo la kutatua changamoto za utoaji wa huduma za kijamii .

Hayo yamesemwa na Askofu wa Makanisa ya God Fellowship Church (GFC) Malaki wakatia akizungumza na Viongozi wa Dini na Serikali ya mtaa katika kijiji cha Chiwe na Mtanana wakati akielezea mpango wa Kanisa hilo na taasisi ya Foundation for hope wenye Lengo la ushirikiano wa Jamii na Kanisa katika huduma za kiroho  na utoaji wa huduma za jamii.

Picha ni wanakwaya wakitumbuiza katika Mkutano huo. Picha na Seleman Kodima

Akizungumza zaidi katika Mkutano wa kanisa la CFC uliofanyika Chiwe Askofu huyo amesema kuwa kama ilivyokuwa kwa Masia Yesu kristo alivyokuwa akiwaponya wagonjwa ndivyo lengo la Kanisa hilo kuwaponywa watu katika huduma nyingi .

Sauti ya Askofu wa Makanisa ya God Fellowship Church (GFC)

Kwa upande mwingine amesema huduma za kijamii zinazotolewa na Kanisa hilo zinalengo la  jamii nzima pasina kutazama udini,ukabila .

Sauti ya Askofu wa Makanisa ya God Fellowship Church (GFC)