Dodoma FM

Jamii yatakiwa kujitokeza kusaidia malezi

5 February 2024, 6:47 pm

Picha ni bi Hadija Kissa Afisa ustawi wa jamii mwandamizi kutoka wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu.Picha na The morning power show.

Kuna watoto wengi kwenye wanapitia changamoto ya kupata malezi inayotokana na ugumu wa maisha pamoja na wengine kukosa wazazi.

Na Fred Cheti.
Wito umetolewa kwa jamii kujitokeza kusaidia katika malezi kwa watoto wenye uhitaji wa huduma hiyo kwa kuwachukua na kuwapatia malezi ya kambo au kuwaasili ili kuwasidia kupata malezi bora kama watoto wengine.

Wito huo umetolewa na bi Hadija Kissa Afisa ustawi wa jamii mwandamizi kutoka wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu wakati akizungumza katika kipindi cha The Morning Power Show ambapo amesema kuna watoto wengi kwenye wanapitia changamoto ya kupata malezi inayotokana na ugumu wa maisha pamoja na wengine kukosa wazazi.

Sauti ya Bi . Hadija Kissa.

Aidha Afisa Ustawi huyo hapa anaeleze ni hatuaa zipi anaapswa kufuata mtu anaehitaji kupata mtoto kwa ajili ya kumpatia malezi ya kambo au kumuasili na kumpa malezi ya kudumu

Sauti ya Bi . Hadija Kissa