Dodoma FM

Wananchi wahimizwa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa

9 January 2024, 11:38 pm

Picha ni wakazi wa Mtaa wa Chihikwi wakiwa katika mkutano huo na mkuu wa Wilaya . Picha na Thadei Tesha.

Uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa serikali za mitaa unatarajia kufanyika mwaka huu huku wananchi wakiendelea kusisitizwa suala la kushiriki katika kuchagua viongozi sahihi.

Na Thadei Tesha.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma mh. Jabir Shekimweri amewataka wananchi jijini Dodoma kushiriki kikamilifu katika kuwachagua viongozi mbalimbali katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu.

Mkuu wa wilaya ameyasema hayo wakati akiuzungumza na baadhi ya wananchi katika eneo la chihikwi ambapo amesema kuwa ni wakati wa wananchi kushiriki katika kuwachagua viongozi sahihi watakaoweza kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii.

Sauti ya mh. Jabir Shekimweri.
Picha ni muonekano wa mtaa wa Chihikwi jijini Dodoma . Picha na Thadei Tesha.

Dodoma FM imefanya mahojiano na baadhi wa wananchi jijini hapa juu ni kwa namna gani wameweza kujiandaa kushiriki  katika uchaguzi wa serikari  za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu  ambapowanasema kuwa ni vyema wananchi kujitokeza katika zoezi la kupiga kura.

Sauti za wananchi.