Dodoma FM

TMDA yakabidhi dawa na vifaa tiba kwa mkuu wa Gereza la Msalato

16 May 2023, 6:00 pm

Meneja wa TMDA kanda ya Kati Bi. Sonia Henry Mkumbwa na  Mkuu wa Magereza Msaidizi na Mganga wa Zahanati ya Gereza la Msalato, Mrakibu wa magereza Dkt. Abuusalami Mpamba wakikabidhiana vifaa tiba hivyo. Picha na Seleman Kodima.

Vifaa tiba na Dawa zilizokabidhiwa leo na TMDA vimetokana na  kaguzi zilizofanywa na Mamlaka hiyo na kuondosha katika soko la dawa  ambayo vinafaa kwa matumizi lakini kwa mujibu wa sheria ya dawa na vifaa tiba ,dawa havikupaswa kuuzwa ama kutumika katika maeneo husika .

Na Seleman Kodima.

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba kanda ya kati TMDA leo imekabidhi Vifaa tiba na Dawa  vyenye thamani ya shilingi Milioni 15 .599  kwa Mkuu wa Gereza la Msalato ili viweze kutumika katika zahanati ya gereza la Msalato.

Makabidhiano hayo  yamefanyika katika zahanati ya Gereza la Msalato  na Meneja wa TMDA kanda ya Kati BI Sonia Henry Mkumbwa na  Mkuu wa Magereza Msaidizi na Mganga wa Zahanati ya Gereza la Msalato ,Mrakibu wa magereza Dkt Abuusalami Mpamba ikiwa ni muendelezo wa  TMDA Kanda ya Kati ikiendelea na utekeleza majukumu yake lengo likiwa ni kulinda afya ya jamii.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Meneja wa TMDA kanda ya kati Bi Sonia amesema kuwa hatua ya kutoa msaada huo ni baada ya kakugizi walizofanya awali na kuona hali ya miundombinu ya zahanati ,wahudumu ,mfumo wa utunzaji wa nyaraka.

Sauti ya Meneja wa TMDA kanda ya kati Bi Sonia .

Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Msaidizi na Mganga wa Zahanati ya Gereza la Msalato ,Mrakibu wa magereza Dkt Abuusalami Mpamba  akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Gereza na  Kamishina  jenerali wa Magereza Tanzania amesema kuwa kupitia dawa hizo watahakikisha zinawafikia walengwa ili kuwatibu na kuwaponya.

Sauti ya Mkuu wa Magereza Msaidizi na Mganga wa Zahanati ya Gereza la Msalato
Baadhi ya dawa zilizo kabidhiwa na TMDA kwa Zahati hiyo. Picha na Seleman Kodima.

Nao baadhi ya Wanajamii wanaopata huduma katika Zahanati hiyo akiwemo Anjela Kimario,Prisca Paulo na Ovidio Francis  wamesema msaada huo utakuwa tumaini la upatikanaji zaidi wa dawa na vifaa tiba na itapunguza changamoto  kwenye huduma za msingi za Mama na Mtoto.

Sauti za wanajamii.