Dodoma FM

Utabiri wa hali ya hewa unavyosaidia wakulima Hombolo

14 December 2020, 2:56 pm

Wakulima katika Kata ya Hombolo Bwawani jijini Dodoma wakiwa shambani wakipanda mbegu

Na,Mindi Joseph,

Dodoma.

Utabiri wa hali ya hewa nchini umetajwa kuwasaidia wakulima katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi yanayojitokeza katika msimu wa Kilimo.
Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya wakulima katika kata ya Hombolo jijini Dodoma wamesema kuwa utabiri huo unaotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA umewasaidia kujua namna ya kukabiliana na mabadiliko hayo na aina ya mbegu zinazoendana na hali ya hewa itakayokuwepo.
Wameongeza kuwa bado kuna changamoto ya baadhi ya wakulima kutokupata taarifa hizo kutokana na mazingira wanayoishi hususani Maeneo ya pembezoni mwa mji.

Naye Afisa Kilimo wa Kata ya Hombolo Bwawani Bwawani Bw.Pascal chuba sabunyoni amesema Katika msimu huu wa kilimo wanafanya jitihada kuhakikisha Elimu ya mabadiliko ya tabianchi inawafika wakulima kupitia mikutano ya hadhara.

Wakulima Kata ya Hombolo Bwawani wakipanda mbegu kwa kutumia kamba

Aidha Utabiri wa Hali ya hewa unachambua athari za hali ya hewa iliyojitokeza na inayotarajiwa kwenye mazao wakati huohuo mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri ukuaji wa maendeleo ya mimea lakini pia ubora wa mavuno, ufanisi wa nyenzo za kilimo.