Dodoma FM

Mabadiliko ya bei kuongeza upatikanaji wa maji Dodoma

15 August 2023, 9:55 am

Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph,akitoa elimu kwa Wananchi wakati wa kikao cha kukusanya maoni ya wananchi kuhusu maombi ya kurekebisha bei za huduma za Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA). Picha na Mzalendo.

Ongezeko hilo la bei za maji limechangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya kiuchumi duniani.

Na Selemani Kodima.

Baada ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Kuweka wazi mabadiliko ya bei za huduma za maji zitakazoanza kutumika mwezi August mwaka huu ,Inaelezwa kwa mabadiliko hayo ambayo yatatekelezwa  kwa miaka mitatu yasaidia kuongeza hali ya Upatikanaji wa maji mkoani Dodoma.

Hayo yamesemwa Leo na  Mkuu wa Kitengo cha Mipango ,Tathimini na Ufuatiliaji (DUWASA)Jonathan Shenyagwa  wakati akizungumza katika kipindi cha Dodoma Live kuhusu mabadiliko ya bei mpya za huduma za maji ambapo amesema kupitia Bei hizo kwa asilimia 90 wanategemea kupunguza Tatizo la Mgao wa maji katika jiji la Dodoma.

Sauti ya Jonathan Shenyagwa .

Akizungumza kuhusu Ankara mpya ,zenye mabadiliko ya Bei za huduma ya Maji,Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Bi ,Lena Mwakisale amesema bei mpya zitaanza kutumika mwishoni mwa mwezi huu ,tarehe 24  Agosti ambapo mabadiliko  hayo yameongezeka kidogo.

Amesema ukitazama kwenye kila kundi la Wateja kilichoongeza ni Shilingi 200  kwa kila unit ambapo kwa Wateja wa Majumbani itakuwa Shilingi 1510 ,Wateja wa Taasisi 1880,Wateja Biashara 1930 ,Wateja Viwanda 1930 ,wateja wa Magati 1000 na Wateja wa Jumla 2000.

Amesema kwa Mwaka 2024/2025 itakuwa tofauti ambapo Wateja wa Majumbani itakuwa Shilingi 1650 ,Wateja wa Taasisi 2050 ,Wateja Biashara 2100,Wateja wa Viwandani 2100 na Wateja Wakubwa 2060

Sauti ya Bi ,Lena Mwakisale.

Kwa upande Mwingine Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Tathimini na Ufuatiliaji Bw Shenyangwa amesema baada ya Mabadiliko  hayo ya bei ,DUWASA ina  mkakati kutoa Huduma endelevu kwa wakazi wa Dodoma  na kupitia miradi  inayotekelezwa ya uchimbaji wa Visima vya maji katika maeneo ya pembezoni itaongeza hali ya upatikanaji wa maji jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph,akitoa elimu kwa Wananchi wakati wa kikao cha kukusanya maoni ya wananchi . Picha na Mzalendo.

Amesema moja ya Mradi unaotegemewa kuongeza hali ya Uzalishaji wa maji katika maeneo ya jiji la Dodoma ni pamoja na mradi wa visima vya Maji nzuguni ambao upo hatua za Mwisho kukamilika ili kuanza  kutoa maji.

Mkuu wa Kitengo cha Mipango ,Tathimini na Ufuatiliaji (DUWASA)Jonathan Shenyagwa  wakati akizungumza katika kipindi cha Dodoma Live .Picha na Emmanuel Munishi.

Kwa mujibu wa EWURA imetaka kila Mamlaka kupitia bei zake kila baada ya miaka Mitatu na DUWASA haikua imefanya hivyo katika kipindi hicho huku moja ya sababu ilitojwa kusukuma mabadiliko hayo ni kuwezesha Mamlaka kumudu gharama za uendeshaji, kuongeza ufanisi wa DUWASA katika utoaji wa huduma bora, kuimarisha na kuboresha usalama wa maji yanayozalishwa na kusambazwa.