Dodoma FM

Ubadilishaji wa miundombinu ya maji taka umefikia asilimia 80

21 February 2023, 12:31 pm

Mkurugenzi wa huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira Mhandisi Emmanuel Mwakabole.Picha na Martha Mgaya

Ubadilishaji wa miundombinu ya maji taka katika Eneo la Area C na D Mkoani Dodoma umefikia asilimia 80.

Na Mindi Joseph.

Ubadilishaji wa miundombinu ya maji taka katika Eneo la Area C na D Mkoani Dodoma umefikia asilimia 80, hizi ni jitihada za kuendelea kukabiliana na Changamoto ya miundombinu ya maji taka ambayo imekuwa na kikwazo kwa wakazi wa maeneo mbalimbali.

Mifumo ya maji taka inahudumia asilimia 20 ya wakazi wa Dodoma, Dodoma TV imefanya mahojiano na Mkurugenzi wa huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira Mhandisi Emmanuel Mwakabole.

Sauti ya Mhandisi Emmanuel Mwakabole.

Mitaa ya Area C na D ni mitaa mikongwe katika jiji la Dodoma lakini ilikuwa inatumia mfumo wa maji taka wa zamani toka mwaka 1978.