Dodoma FM

Miaka 65 ya ndoa: Wafariki na kuzikwa siku moja

23 May 2023, 3:52 pm

Matukio katika picha ni baadhi ya waombolezaji wakiwa katika mazishi wa wapendanao hao. Picha na Bernad Magawa.

Tukio hilo la aina yake limewatafakarisha watu wengi maeneo hayo huku wengine wakidai ni msiba wa aina yake ambao umevuta hisia za watu wengi na kuweka historia kwa waombolezaji waliofika msibani hapo.

Na. Bernad Magawa .

Katika hali ambayo si ya kawaida kutokea, wanandoa wawili wilayani Bahi wamefariki dunia kwa siku moja baada ya kuugua kwa muda mrefu na kuzikwa siku moja baada ya kudumu katika ndoa kwa takribani miaka 65 huku wakiacha watoto 9, wajukuu 20 na vitukuu 24.

Wanandoa hao Blez Muhumpa 95 na Martina Lyati 94 ambao walifariki dunia Mei 21na kuzikwa Mei 22, 2023 wameweka historia ambayo inasemekana kuwa haijawahi kutokea ambapo Bi. Martina Lyati alitangulia kufariki majira ya saa 4 kamili asubuhi na kufuatiwa na mumewe nusu saa baadaye.

Paroko wa parokia ya Bahi Padri Levokatus Majuto akizungumza katika ibada ya mazishi ya marehemu hao ambao walipendana katika maisha yao yote amewaasa wanadamu kuwa karibu na Mungu na kujiweka tayari muda wote kwani Mungu humwita mtu wakati wowote.

Sauti ya Padri Majuto.
Matukio katika picha ni baadhi ya waombolezaji wakiwa katika mazishi wa wapendanao hao. Picha na Bernad Magawa.

Awali akisoma historia ya marehemu hao mmoja wa wajukuu wao alisema wazee hao waliugua kwa muda mrefu na kupata tiba maeneo mbalimbali bila kupata nafuu.

Sauti ya Mjukuu wa marehemu.