Dodoma FM

NGO’S zatakiwa kufanya tathmini za mazingira

24 October 2023, 1:38 pm

Picha ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma akizumza jana ofisini kwakwe.Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Kikao hicho kimefanyika hapo jana ofini kwake ambapo katibu tawala alizungumza na wadau hao.

Na Mariam Kasawa.
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) yanayojihusisha na masuala ya Mazingira kukutana na kufanya tathmini ya namna Utunzaji Mazingira unavyotekelezwa Jijini Dodoma kwa kila robo ya Mwaka wa Fedha.

Bw. Gugu amesema hayo katika kikao kazi cha Utunzaji wa Mazingira kwa mashirika hayo yaliyopo Mkoani Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jengo la Mkapa.

Sauti ya Mh. Ally Gugu.