Shekimweri aongoza mbio za pole kuuenzi mwenge wa uhuru
15 June 2026, 16:29

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Waandamizi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma, Shadaiya Hassan, alisema kuwa mbio hizo zimeandaliwa kwa lengo la kuendelea kuuenzi Mwenge wa Uhuru na kuhamasisha wananchi kuishi falsafa zake hata baada ya mbio za Mwenge kupita wilaya ya Dodoma.
Na Mariam Kasawa.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri ameongoza mbio za pole za KM 5 za kuuenzi Mwenge wa Uhuru zilizoanzia Ofisi ya Afisa Tarafa Dodoma Mjini na kuhitimishwa katika Uwanja wa Mtekelezo.
Akizungumza wakati wa mbio hizo, Alhaj Shekimweri alimshukuru Afisa Michezo wa Jiji la Dodoma, Neema kilongola kwa kuratibu mbio hizo za pole zilizokutanisha makundi mbalimbali ikiwemo Skauti, Karate na waandamizi waliowahi kushiriki mbio za Mwenge wa Uhuru.
Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru unahimiza uzalendo na kudumisha mshikamano.