Dodoma FM
Dodoma FM
9 September 2025, 2:21 pm

Afisa Mhifadhi Daraja la Kwanza ambaye pia ni Daktari wa Wanyamapori Masalu Makoye Mroje, amesema simba huyo atasafirishwa kwenda eneo la mbali lenye mazingira rafiki, ili kuzuia madhara kwa wananchi na mifugo yao.
Na Peter Mnunduma.
Mamlaka ya Usimamizi waWanyamapori Tanzania (TAWA) imefanikiwa kumkamata samba jike akiwa hai baada ya mfululizo wa mashambulizi ya wanyama na kuua zaidi ya mifugo 20 katika wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma.
Simba huyo aliingia kwenye rada za askari wa TAWA majira ya saa 4 usiku, Septemba 6, 2025, katika kijiji cha Chemchem, kufuatia msako mkali uliodumu kwa siku tatu ambapo mnyama huyo alijikuta tayari amenasa katika mtego maalum uliowekwa naAskari hao.
Imeripotiwa kuwa Simba huyo amekuwa akifanya mashambulizi ya mifugo katika vijiji vya Chemchem na Iyoli, kata ya Kingale ambapo katika nyakati tofauti waliua ng’ombe wawili na punda mmoja na baadae kuua ng’ombe 18 katika gereza la King’ang’a.

Aidha, waliripotiwa pia kuua mbuzi wawili katika kijiji cha Iyoli.
Kutokana naongezeko la matukio hayo, mamlaka ilianza operesheni ya kudhibiti simba hao kwakutumia askari wake na baadaye kuongeza timu ya madaktari wawanyama. Hatimaye, mnamo Septemba 6 majira ya saa 4 usiku, samba jike alikamatwa kwa kutumia mbinu za kitaalamu.
Kwa upande wao, wananchi wa Kijiji cha Chemchemi, Kata yaKingale, wilayani humo, wameipongeza serikali kupitia TAWA kwa uwajibikaji wake katika kukabilia na changamoto za wanyamapori waharibifu, hususan kitendo cha kumdhibiti simba huyo aliyezua taharuki kwa wananchi.