Dodoma FM

Wananchi Ihumwa wakumbwa na hofu mikopo holela

18 May 2026, 13:09

Wakazi hao wamewaomba viongozi kuwafuatilia wadau hao wa mikopo ili waje watoe ufafanuzi.Picha na Mtandao.

Wananchi wamejikuta wakitumia gharama zao kufungua accaunt bank ili kupata mkopo huo na hadi sasa hawaelewi chochote kuhusu mkopo huo.

Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Mtaa wa Ihumwa A jijini Dodoma wamegubikwa na hofu ya kutapeliwa baada ya kujitokeza wawezeshaji waliodai wanatoa mikopo Kwa vikundi vya vijana.

Wakiongea na Taswira ya habari baadhi ya wakazi wa mtaa huo wameiomba serikali ya mtaa na viongozi wa kata kuingilia kati suala hilo kwani wananchi wamejikuta wakitumia gharama zao kufungua accaunt bank ili kupata mkopo huo na hadi sasa hawaelewi chochote kuhusu mkopo huo.

Wakazi hao wamewaomba viongozi kuwafuatilia wadau hao wa mikopo ili waje watoe ufafanuzi kwa wananchi kuwa ni hatua gani zinafuata baada ya wananchi kufungua accaunti hizo.

Sauti za wakazi .

Aidha wameiomba Serikali ya mtaa huo kuwa makini na wageni wanaoingia mitaani kwaajili ya shughuli mbalimbali na kuwafungulia wananchi accaunt bila maelezo ya kutosha huku wageni hao wakituhumiwa kuwafungulia accout hadi wanafunzi bila ridhaa za wazazi wao.

Sauti za Wakazi

Lazaro Chiswagala katibu Kata wa chama Cha Mapinduzi Kata ya Ihumwa amekiri uwepo wa mchakato huo ambao amesema mchakato huo ulikuwepo na hauna majibu rahisi kwa wananchi hivyo watafuatilia ili kutatua suala hilo.

Sauti ya Lazaro Chiswagala.

Naye Afisa maendeleo wa Kata hiyo ya Ihumwa Bi. Anna Masijita amepiga marufuku wananchi kujihusisha na ufunguajia wa akaunti kiholela pasipo kuwa na taarifa kamili zinazohusisha taasisi hiyo na Serikali ya mtaa au Kata .

Sauti ya Bi. Anna Masijita.