Dodoma FM

NEMC yafanya operesheni vifungashio visivyo na ubora.

21 April 2021, 10:04 am

Na; Mindi Joseph.

Baraza la  Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati Dodoma limefanya operesheni ya ukaguzi wa vifungashio visivyokidhi ubora sokoni na kukamata vifungashio takribani kilo 125 na kuvitaifisha.

Akizungumza na taswira ya Habari baada ya kufanya ukaguzi huo Mratibu wa uzingatiaji na utekelezaji wa sheria ya mazingira NEMC kanda ya katimhandisiBoniphance Paul Guni amebainisha kuwa katika zoezi hilo jumla ya watuhumiwa 8 wamekutwa na vifungashio hivyo na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha mhandisi Boniphance amewataka wale wote wanaondelea kutumia vifungashio visivyokidhi matakwa kuvisalimisha katika ofisi za baraza la mazingira NEMC na hawatachukuliwa hatua zozote badala yake vitateketezwa.

Kwa upande wake Mkaguzi wa shirika la Viwango Tanzania kanda ya kati Dodoma Domisiano Rutahala amesema kuwa TBS imebaini uwepo wa baadhi ya wazalishaji wa vifangashio ambao wamekiuka makubaliano ya awali na wamepanga kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na wanaoghushi nembo ya Tbs.

Naye John Tarimo ambaye ni mfanyabiashara wa soko la Sababsaba ni miongoni mwa watu nane waliokamatwa na vifungashio visivyokidhi ubora na kutozwa faini ya laki moja,  amewataka wananchi kutotumia vifungashio hivyo ili kuendelea kutunza mazingira kwa vizazi vijavyo.

Zoezi la ukaguzi wa vifungashio visivyokidhi viwango ni endelevu katika sehemu zote na litaendelea katika mikoa ya Singinda na Tabora ili kulinda miundombinu ya maji safi , shughuli za kilimo, pamoja na kuwalinda wanyama.