Dodoma FM

Mpango maalum ‘Tumewasikia Tumewafikia’ wazinduliwa Dodoma

2 November 2023, 12:46 pm

Picha ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh Nape Nnauye akiongea katika uzinduzi huo. Picha na Thadei Tesha.

Mpango huo ulizinduliwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma ambapo ni programu ya nchi nzima yenye lengo la kuhakikisha wananchi wanapata taarifa juu ya yale yanayotekelezwa na seikali ya awamu ya sita ukiwa na jina TUMEWASIKIA TUMEWAFIKIA.

Na Thadei Tesha.

Uzinduzi wa mpango maalum ulioandaliwa na idara ya habari maelezo yenye jina la TUMEWASIKIA TUMEWAFIKIA umezinduliwa  novemba 1jijini Dodoma.

Huu ni mpango wa nchi nzima wenye lengo la kuhakikisha wananchi wanapata taarifa juu ya yale yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita

Akizungumza wakati wa kuzindua programu hiyo waziri wa habari mawasiliano na teknolojia ya habari Mh Nape Nnauye amasema kuwa mpango huo uliozinduliwa jijini dodoma ni mpango wa nchi nzima wa kuhakikisha wananchi wanapata taarifa kupitia idara ya habari maelezo huku akiwataka wananchi pamoja na viongozi wa serikali za mitaa kutoa ushirikiano katika suala la kutoa taarifa.

Sauti ya Mh Nape Nnauye.
Picha ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh Rosemery Senyamule akiongea katika mkutano huo.Picha na Thadei Tesha.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh Rosemery Senyamule pamoja na mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw John Kayombo hapa wanatumia fursa hii kuelezea maendeleo na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofanywa na serikali ya awamu ya sita katika jiji la Dodoma.

Sauti za Mh Rosemery Senyamule pamoja na mkurugenzi Bw John Kayombo

Akizungumza wakati wa kuhitimisha hafla ya uzinduzi huo Naibu Waziri Ofisi ya rais TAMISEMI Mh. Festo Dugange ametoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuwa na maafisa habari ili kurahisisha lengo la mpango huo.

Sauti ya Mh. Festo Dugange.
Picha ni mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw John Kayombo akiongea katika mkutano huo. Picha na Thadei Tesha.