Dodoma FM

Tanzania kunufaika na mpango wa Grand Challenges

4 June 2026, 18:26

Picha ni Naibu waziri wa elimu Bi Wanu Hafidh Ameir leo Jijini Dodoma alipokuwa  akizindua mpango wa uendelezaji tafiti na ubunifu nchini (GRAND CHALLENGES TANZANIA).Picha na Picha na GC-TZ.

Akiongea katika hafla ya uzinduzi huo katibu mkuu ofisi yapili ya makamu wa Rais Zanzibar Dkt. Islam Seif amesema mpango huu wa Grand Challenges Tanzania utaleta maarifa ya kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto za afya, kijamii, mazingira, ukosefu wa chakula na nyinginezo.

Na Mariam Kasawa.

Imeelezwa kuwa Tafiti na Bunifu ni nyenzo kuu ya kukuza uchumi na maendeleo nchini.

Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa elimu Bi Wanu Hafidh Ameir leo Jijini Dodoma alipokuwa  akizindua mpango wa uendelezaji tafiti na ubunifu nchini (GRAND CHALLENGES TANZANIA) amesema mpango huu utasaidia kuleta suluhisho la mahitaji mbalimbali yanayo zikabili jamii hapa nchini.

Sauti ya Mh.Wanu Hafidh Ameir

Aidha amesema mawanda mapana ya mpango huu yanaendana na mpango wa maendeleo hapa nchini hivyo mpango huu utawezesha kuonesha maeneo maalum kwa maendeleo.

Sauti ya Mh.Wanu Hafidh Ameir

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu costech Dkt. Amos Nungu amesema hii ni fursa kwa watafiti watanzania kushiriki na kupata ushirikiano na wadau wengine .

Amesema program hii ni endelevu ambapo kwa awali  inazinduliwa kwa miaka mitano .

Sauti ya Dkt. Amos Nungu