Dodoma FM

Ligi kuu Tanzania Bara kurejea dimbani April 8

31 March 2021, 12:26 pm

Na; Matereka Junior.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania,(TPLB) Almas Kasongo amesema kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea Aprili 8 baada ya kutimiza siku 21 za maombolezo.

Amesema baada ya kuipitia ratiba yao wamekuja na mabadiliko ambapo ligi inarejea tarehe 8, 9 na 10 Aprili, michezo ya tarehe 6 na 7 itachezwa tarehe 9-10 michezo iliyopaswa kuchezwa tarehe 10 ipo palepale.

Kasongo anasema ligi itaendelea tarehe 8, 9 na 10 itakuwa michezo ya awali ya kufungua ligi kutoka pale ambapo walisimama kwa siku 21 za maombolezo.

Nae Meneja wa Dodoma Jiji, Onesmo Lubeleje amezungumzia ratiba ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Prisons, ambapo amesema wao ratiba wameipokea vema kwasabubu imetoa muda mzuri wa kuwafuata Prisons.

Lubeleje ameongeza kuwa, Sumbawanga Rukwa ni mbali hivyo kutoka leo hadi tarehe 10 wamepata muda mzuri wa kusafiri kuwafuata na baada ya hapo watarejea Dodoma kuwasubiri Namungo April 18.