Dodoma FM

Wakulima watakiwa kuendelea na shughuli za kilimo bila kuhofia mvua

9 February 2022, 2:58 pm

Na; Benard Filbert.

Licha ya mvua kuwa chini ya wastani msimu huu imeelezwa bado kuna uwezekano mkubwa wa kupata mazao yakutosha kwa wakulima wa mazao mbalimbali kanda ya kati.

Hayo yanajiri kufuatia baadhi ya wakulima kuwa na wasiwasi wa kupata mazao chini ya kiwango kwa kile kinachodaiwa msimu huu mvua kunyesha chini ya wastani.

Hassan Kiseto ni mkuu wa idara ya kilimo mji wa Kondoa mkoani Dodoma ameiambia taswira ya habari licha ya mvua kuwa chini ya wastani msimu huu hakuna wasi wasi kwa wakulima juu ya mavuno na hivyo waendelee na shughuli za kilimo kama kawaida.

Kadhalika amesema kuwa kwa wale wakulima ambao bado hawajapanda mahindi hadi hivi sasa ni vyema wakaagalia mbegu zinazokomaa kwa muda mfupi kuendana na taarifa za mvua kwa msimu huu.

Wakulima wanasisitizwa kuwa karibu na wataalamu wa kilimo ili kupata taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa ili kufanya kilimo chenye tija.