Dodoma FM

EWURA yatoa leseni kwa zaidi ya mafundi umeme 5000

9 August 2023, 6:28 pm

Afisa huduma kwa wateja EWURA akizungumza na Dodoma Tv. Picha na Mindi Joseph.

EWURA imeendelea kuwakumbusha Mafundi Umeme kufanya kazi kwa mujibu wa kanuni za Umeme hususani kanuni namba 15, 16 na 17.

Na Mindi Joseph.

Zaidi ya mafundi umeme 5000 wamepatiwa leseni na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ili kulinda usalama wa mali na uhai.

Juma Singano ni Afisa huduma kwa wateja EWURA anasema kanuni na taratibu za kuomba Leseni Mafundi umeme wanazifahamu.

Sauti ya Afisa huduma kwa wateja EWURA.

Mhandisi Nicoulas Kayombo kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Kanda ya kati Dodoma amesema lengo la utoaji wa leseni kwa mafundi umeme ni kufanya kazi kwa usahihi, uhakikika na usalama.

Mhandisi Nicoulas Kayombo kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Kanda ya kati Dodoma.Picha na Mindi Joseph.

Hadi sasa zaidi ya mafundi 5000 wamesajiliwa na kupewa leseni ili waweze kufanya kazi kwa uhakika.

Sauti ya Mhandisi Nicoulas Kayombo .