Dodoma FM

Waganga tiba asili, wakunga 28 watunukiwa vyeti

3 July 2023, 2:50 pm

Kamishna wa kamisheni ya polisi jamii CP Faustine Shilogile akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo. Picha na Alfred Bulahya.

Mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa wiki moja yametolewa na wakufunzi kutoka Taasisi ya afya na sayansi shirikishi Dodoma (DIHAS) (Dodoma Institute of Health and allide Science).

Na Alfred Bulahya.

Jumla ya waganga wa tiba asili na wakunga 28 kutoka mikoa tofauti nchini wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya kuinua ubora wa tiba asili na tiba mbadala ngazi ya cheti, yaliyoandaliwa na serikali kupitia wizara ya afya.

Akifunga mafunzo hayo Julai mosi jijini Dodoma Kamishna wa kamisheni ya polisi jamii CP Faustine Shilogile, amewataka wahitimu hao kuwezesha ulinzi wa afya za wananchi kwa kuhakikisha anatoa huduma kwa kufuata kanuni na miongozo inayotolewa na wizara ya Afya.

Sauti ya Kamishna wa kamisheni ya polisi jamii CP Faustine Shilogile.
Kamishna wa kamisheni ya polisi jamii CP Faustine Shilogile akiwatunuku vyeti wahitimu wa mafunzo hayo. Picha na Alfred Bulahya.

Katibu wa umoja wa waganga wa tiba asili na wakunga Tanzania (UWAWATA) Lucas Mlipu akaliomba jeshi la polisi nchini kushirikiana na waganga hao katika kuwafichua baadhi yao ambao wamekuwa wakichufua taswira ya waganga hao.

Sauti ya Katibu wa umoja wa waganga wa tiba asili na wakunga Tanzania.

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wameenza namna mafunzo hayo yatakavyosaidia kuboresha huduma zao.

Sauti za baadhi ya wahitimu.