Dodoma FM

Serikali yaombwa kufanyia mabadiliko sheria ya mtandao

23 June 2022, 2:33 pm

Na;Mindi Joseph .

Serikali imeombwa kufanya mabadiliko katika sheria ya Mtandao ambayo imetajwa kuwa na mapungufu na kuchangia watu kuchapisha na kutuma taarifa za watu mtandaoni pasipo kuwa na idhini ya wahusika.

Taswira ya habari imezungumza na Mwanasheria kutoka Taasisi ya Zaina foundation Neema Oledemulo amesema kuna haja ya serikali kuangalia  sheria hii na kuifanyia marekebisho.

Ameongeza kuwa Uelewa wa sheria kwa wananchi  bado ni changamoto hali inayochangia watu kutuma taarifa na kuchapisha pasipo kujua kuwa ni kosa kisheria.

.

Sheria ya Mtandao inatakiwa kufanyiwa maboresho kufuatia ukuaji wa matumizi ya TEHAMA na kuongezeka kwa kasi ya watumiaji wa mitandao.

.

Sheria ya makosa ya kimtandao ilipitishwa na Bunge tarehe Mosi Aprili 2015 na kuidhiniswa na rais wa Tanzaia Aprili, 25 2015 Lakini wadau wameendelea kuomba ifanyiwe maboresho.