Dodoma FM

Wakulima wa Jangwani Laikala walia kukosa mavuno ya alizeti

14 July 2023, 4:44 pm

Eneo la Jangwa linalopatikana kijiji cha Laikala wilayani Kongwa eneo ambalo wakazi wa eneo hilo hulitumia kwa kilimo cha alizeti. Picha na Mindi Joseph.

Zao la alizeti limekuwa maarufu kutokana na mafuta yake kupendwa na watu wengi kwa sababu hayachanganywi na kemikali yoyote na bei yake imekuwa ikipanda na kushuka lakini Mei 29 2023 Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde alisema Serikali ipo mbioni kuanzisha mfuko wa kukabiliana na changamoto ya kuporomoka kwa bei ya alizeti Nchini.

Na Mindi Joseph.

Jangwa la Laikala Wilayani kongwa kwa kiasi kikubwa limewapa hasara wakulima kwa kuteketeza zao la Alizeti Msimu huu.

Wilaya ya Kongwa ni miongoni mwa Wilaya saba zinazounda Mkoa wa Dodoma.

Mkoa ambao umejariwa utajiri mkubwa wa Zao la kimkakati la Alizeti.

Hili hapa ni Jangwa la Laikala liliopo wilayani Kongwa kwa kiasi kikubwa hutumika kwa shughuli za  kilimo cha Alizeti.

Mara nyingi wakulima wanaolima katika Jangwa hili huvuna na wengine hukosa mavuno.

Kutokana na uhaba wa mvua mwaka huu zao la alizeti halikuweza kabisa kuhimili katika jangwa hilo. Picha na Mindi Joseph.

Tazama hili ni shamba ambalo mkulima amelima katika jangwa la laikala msimu huu na hajavuna chochote hii ni kutokana na ukosefu wa mvua za kutosha zinazohitajika kustawisha zao hili.

Sio katika jangwa la Laikala tu Wakulima wa zao la alizeti kwa msimu huu wengi wanalalamiki kuhusu uzalishaji hafifu.