Dodoma FM

Wakulima Kongwa watakiwa kulima kilimo chenye tija

27 October 2022, 10:21 am

Na; Benard Filbert.

Wakulima  wilaya ya Kongwa wamehimizwa kutumia teknolojia ya kisasa yakuvuna maji na kutunza udongo ili kufanya kilimo chenye tija.

Hayo yameelezwa na mkuu wa idara ya kilimo na mifugo wilaya ya Kongwa Bw. wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu hali ya kilimo katika wilaya ya Kongwa.

Amesema moja ya lengo la wilaya ya Kongwa hivi sasa ni kuwataka wakulima kufanya kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia mbalimbali ambazo zitaleta uzalishaji Chanya.

.

Hata hivyo amesema changamoto ya teknolojia za kisasa zinahitaji nguvu ya ziada kitu ambacho sio rahisi kwa kila mkulima.

.

Baadhi ya wakulima wamesema ni vyema wakuu wa Idara za kilimo wakawa wanafika kila sehemu ili kutoa elimu ipasavyo juu ya teknolojia za kisasa.

.

Wakulima nchini wanahimizwa kufuata na kutumia teknolojia za kisasa hali itakayosaidia kufanya uzalishaji wenye tija na kuendana na kilimo cha kisasa.