Dodoma FM

Uhaba wa maji wasababisha migogoro ya ndoa katika kijiji cha Mpakani

5 October 2021, 11:31 am

Na ;Victor Chigwada.

Huduma hafifu ya upatikanaji wa maji safi na salama umekuwa changamoto kwa Wananchi wa kitongoji cha Mpakani Kata ya Kibaigwa Wilaya ya Kongwa hali inayosababisha migogoro ya ndoa

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema wanaiomba Serikali kuboresha huduma hiyo kwani inawalazimu kuamka usiku kwenda kutafuta maji hali inayochochea migogoro ya ndoa

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Bw.Nikolasi Iyanex amekili uchache wa miundombinu iliyopo ambayo inasababisha wanachi kuamka usiku kwaajili ya foleni huku wengine wakilazimika kutembea umbali mref

Naye Diwani wa Kata ya Kibaigwa Bw.Chande Mrisho amesema kuwa licha ya changamoto ya miundombinu lakini tayari wameanza kupunguza adha hiyo kwa baadhi ya maeneo

Mamlaka ya maji ya mji mdogo wa Kibaigwa ndiyo yenye jukumu la kusimamia huduma za maji safi na maji taka kwa wananchi hao