Dodoma FM

Chinuguli waomba kuongezewa Nguzo za umeme

20 December 2023, 3:16 pm

Picha ni nguzo za umeme zikiwa zimerundikwa. Picha na Full shangwe blog.

Licha ya shughuli za ufungwaji wa nyaya za umeme kuendelea katika kijiji hicho  lakini huduma haionekani kuwa rafiki kwa wananchi.

Na Victor Chigwada .                                     

Wananchi wa Kata ya Chinuguli Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kuwaongzea idadi ya nguzo za nishati ya umeme ili kuendana na mahitaji ya wananchi.

Hayo wameyasema wakati wakizungumza na Taswira ya Habari ambapo wamesema kuwa licha ya shughuli za ufungwaji wa nyaya za umeme kuendelea katika kijiji hicho  lakini huduma haionekani kuwa rafiki kwa wananchi.

Wamesema kuwa hali imechangiwa na uwepo wa idadi ndogo ya nguzo za Umeme ambazo nyingi zimeelekezwa kwenye taasisi za kijamii.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Chinuguli  Sanjeli Njerula ameishukuru Serikali kwa jitihada za kuwaunganishia  nishati ya umeme licha ya kuwa haujitoshelezi.

Sauti ya Bw.Sanjeli Njerula.

Nae  Diwani wa Kata hiyo Bw.Mathiasi Mele ameiomba Serikali kuongeza nguvu ya nguzo  za nishati ya umeme kwani idadi ya zilizopo haziwezi kuwanufaisha wananchi wa kijiji hicho

Sauti ya Bw.Mathiasi Mele .