Dodoma FM
22 June 2026, 17:02

Uimara wa vihenge hivi umefanya viwepo hadi leo katika eneo hilo na kufanya eneo hilo kuitwa Vilindoni.
Na Yussuph Hassan.
Historia ya Vilindoni inaonesha kuwa eneo hili limekuwepo kwa muda mrefu kama makazi ya watu waliotegemea kilimo na ufugaji kwa maisha yao ya kila siku. Miongoni mwa alama muhimu za historia yake ni Shule ya Msingi Vilindoni, moja ya taasisi kongwe katika eneo hilo, iliyoanzishwa mwaka 1975.
Inaelezwa kuwa vihenge hivi hata baada ya matumizi ya kutunzia mazao viliendelea kutumika kwa matumizi mengine kama kugeuzwa kuwa ofisi ya kijiji na kituo cha polizi.