Dodoma FM

Maswi awataka watumishi kuwajibika

19 May 2026, 16:46

Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Eliakim Maswi akizungumza wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba jijini Dodoma.Picha na Maendeleo ya jamii.

Pia amewataka watumishi kuwahi kazini na kufanya kazi kwa kujituma, akisisitiza kuwa serikali imewaamini kwa kuwapa nafasi hizo wakati wananchi wengi bado wanatafuta ajira.

Na Elizabeth Tanzania.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Eliakim Maswi, amewahimiza watumishi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii, uwajibikaji na kuongeza ufanisi ili kuboresha utendaji ndani ya wizara.

‎Akizungumza wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba jijini Dodoma, Maswi amesema kila mtumishi anapaswa kutekeleza majukumu yake kwa umakini na kuchangia maendeleo ya Wizara na taifa kwa ujumla.

‎Aidha, amesema pamoja na wizara hiyo kuwa miongoni mwa wizara zinazofanya vizuri nchini, bado baadhi ya watumishi wanahitaji kubadili mtazamo wao wa kazi na kuongeza juhudi katika utekelezaji wa majukumu yao.