Dodoma FM

Wananchi wahofia bidhaa kupanda bei mwezi mtukufu

20 March 2023, 5:35 pm

Hali ilivyo juu ya upatikanaji wa bidhaa za vyakula masokoni.Picha na Martha Mgaya

Baadhi ya wananchi jijini dodoma wameeleza namna hali ilivyo juu ya upatikanaji wa bidhaa za vyakula masokoni kuelekea mwezi wa ramadhani.

Na Thadei Tesha.

Kuelekea maandalizi ya mwezi mtukufu wa ramadhani baadhi ya wananchi jijini dodoma wameeleza namna hali ilivyo juu ya upatikanaji wa bidhaa za vyakula masokoni.

Hapa ni katikati ya jiji la dodoma nakutana na miongoni mwa wananchi na nimeanza kwa kuwauliza hali ipoje katika suala la bei za vyakula hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kuanza kwa mwezi mtukufu wa ramadhani?

Sauti za wafanyabiashara.

Dodoma fm imefika katika masoko mbalimbali jijini Dodoma na kufanya mahojiano na baadhi ya wafanyabiashara kwa upande wao wanazungumziaje upatikanaji wa bidhaa mbalimbali masokoni?

Sauti za wafanyabiashara.

Katika soko la majengo zipo bidhaa ambazo zinaonekana kushamiri hususani bidhaa za viazi lishe ambapo pamoja na kushamiri kwa bidhaa hizo bado hali ya bei si ya kuridhisha.