Dodoma FM

Wawekezaji wakaribishwa Idifu kuanzisha miradi mbalimbali

20 March 2024, 5:42 pm

Uwekezaji huo utasaidia kukuza uchumi wa wananchi wa maeneo hayo na kusaidia kutoa ajira kwa wananchi. Picha na Blog.

Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imekuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ambapo mpango huo umekuwa ukiratibiwa chini ya mradi wa uwezeshaji usalama wa milki za ardhi unao simamiwa na Serikali kwa kushirikiana na Bank ya Daunia.

Na Victor Chigwada.
Diwani wa Kata ya Idifu Bw.Samweli Kaweya amewakaribisha wawekezaji kwenda kuwekeza katika kata hiyo katika miradi mbalimbali.

Akizungumza hali ya uwekezaji ndani ya kata hiyo,Kaweya amesema kuwa ndani ya kata hiyo kipo kiwanda kimoja cha uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na ngozi ambacho kwasasa kina mwekezaji mpya baada ya aliyekuwepo kushindwa kukiendeleza .

Kaweya amekiri uwepo wa maeneo makubwa ya uwekezaji hivyo ni fursa ya wawekezaji kwenda idifu kwa ajili ya uwekezaji.

Amesema kuwa Kupitia uwekezaji huo utasaidia kukuza uchumi wa wananchi wa maeneo hayo na kusaidia kutoa ajira kwa wananchi.

Sauti ya Bw.Samweli Kaweya.

Aidha amewaondoa hofu kuhusu maeneo ya kata hiyo ambayo tayari yamepimwa kwa mujibu wa sheria.

Sauti ya Bw.Samweli Kaweya.