Dodoma FM

Watu wenye ulemavu watakiwa kuripoti vitendo vya ubaguzi ili haki itendeke

4 December 2023, 3:57 pm

Picha ya watu wenye ulemavu. Picha kwa hisani ya Full Shangwe blog.

Maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu huadhimishwa kila ifikapo Desemba 3 ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni “Tuungane kuchukua hatua katika kutoa huduma ili kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu kwa watu wenye ulemavu”

Na Victor Chigwada.

Watu wenye ulemavu wametakiwa  kuacha kukaa kimya pale wanapoona haki haitendeki ili kuleta usawa .

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi alipohudhuria kongamano la watu wenye ulemavu  lililofanyika katika Kata ya Mtumba jijini Dodoma.

Katambi amesema  ni vema  watu wenye ulemavu  kutoa ushirikiano kwa wizara husika ila kuleta suluhu ya mambo yanayojiri na ambayo yalishajadiliwa ili  kupatiwa ufumbuzi.

Sauti ya mh. Patrobas Katambi

Pia amesema kuwa hakuna vikwazo wala sababu zozote zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa sera kwa watu wenye ulemavu

Sauti ya mh. Patrobas Katambi.

Katambi ameongeza kuwa changamoto ya mmomonyoko wa maadili imekuwa ikichangia kwa kiasi kubwa ukatili kwa watu wenye ulemavu.

Sauti ya mh. Patrobas Katambi.