Dodoma FM

Chinuguli waomba kuongezewa nguzo za umeme

5 April 2023, 3:00 pm

Fundi akifanya matengenezo juu ya ngozo ya umeme.Picha na Tanesco .

Wamesema hali hiyo  inatokana na idadi ndogo ya nguzo zilizopo katika kijiji hicho ambazo zimeelekezwa katika Taasisi mbalimbali.

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa Kata ya Chinuguli Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kuwaongezea idadi ya nguzo za nishati ya umeme ili kuendana na mahitaji ya wananchi

Hayo wameyasema wakati wakizungumza na Taswira ya habari kuhusu hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme kijijini hapo ambapo wamesema kukuwa licha ya shughuli za ungwanishwaji wa  nyaya za umeme kuendelea katika kijiji chao  lakini huduma haionekani kuwa rafiki kwa wananchi

Sauti za wananchi
Fundi akifanya matengenezo juu ya ngozo ya umeme.Picha na Tanesco .

Akizungumza Changamoto hiyo Mwenyekiti wa kijiji hicho Sanjeli Njerula  ameishukuru Serikali kwa jitihada hizo za kuwafungia nishati ya umeme katika kijiji chao licha ya kuwa haujitoshelezi .

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji hicho Sanjeli Njerula

Kwa upande wake  Diwani wa Kata hiyo Bw.Mathiasi Mele ameiomba Serikali kuongeza nguvu katika nguzo  za nishati ya umeme kwani idadi ya zilizopo haziwezi kuwanufaisha wananchi wa kijiji hicho

Sauti ya Diwani wa Kata hiyo