Dodoma FM

Ubakaji, ulawiti kwa watoto wakithiri Dodoma

13 November 2023, 4:31 pm

Asilimia 40 ya wanaofanya ukatili huo ni ndugu familia za watoto hao ,na Huku wengine wakifanyiwa ukatili huo na watu wa karibu na familia zao.Picha na Full shangwe blog.

Ripoti hiyo ni kwa mujibu wa Kituo cha One stop center kwa mwezi Septemba 2023 ambapo takwimu zimebainisha kuwa mkoa wa Dodoma matukio ya ukatili wa kijinsia kwa  watoto 130  kwa matukio ya ubakaji huku watoto 69 wakilawitiwa.

Na Seleman Kodima.

Inaelezwa kuwa wastani wa watoto sita  hadi saba kwa wiki  wanafanyiwa vitendo vya ukatili wa kingono hasa ubakaji na ulawiti.

Hayo yamesemwa na Afisa Ustawi mkoa wa Dodoma Josephine Mwaipopo, wakati akizungumza na wazazi na walezi katika mahafali ya Pre- Unit shule ya Morning Stars ambapo amesema hali ya ukatili kwa mwezi wa tisa inatoa tafsiri ya matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto kuongezeaka.

Amesema watoto wanaothirika zaidi katika ripoti hiyo ni kundi lenye umri wa miaka mitano hadi tisa ambapo walifanyiwa ukatili wa kingono kwa kulawitiwa wakiwa ni wakiume .

Sauti ya Josephine Mwaipopo.
Hali ya ukatili kwa mwezi Septemba inatoa tafsiri ya matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto kuongezeka. Picha na wiki Elimu.

Amesema umri huo umekuwa na  takwimu kubwa ambapo watoto 77 walifanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia huku watoto wa kuanzia umri wa miaka kumi hadi kumi  na nne, watoto 24 walibakwa huku wa kiume 22 wakilawitiwa.

Sauti ya Josephine Mwaipopo.

Akizungumzia wanaohusika na vitendo hivyo kwa mujibu wa ripoti hiyo amesema asilimia 40 ni ndugu familia za watoto hao huku wengine wakifanyiwa ukatili huo na watu wa karibu na familia zao.

Sauti ya Josephine Mwaipopo.