Wanufaika mikopo ya asilimia 10 watakiwa kurejesha kwa wakati
1 June 2026, 16:56

Kasanduka ameongeza kuwa hivi karibuni amepokea barua kutoka Halmashauri inayo eleza deni la zaidi ya Milioni hamsini.
Wito umetolewa Kwa makundi ya wanawake na vijana kuhakikisha wanarejesha mikopo yao kwa wakati ili kutoa fursa kwa vikundi vingine ambavyo havijapata mikopo kunufaika na mkopo huo.
Akiongea na makundi mbalimbali katika kata ya Ihumwa mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Bw John Kasanduku amesema kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya makundi hususani vijana kutopata mikopo kwa wakati hivyo amewaomba wanao pata mikopo hiyo wajitahidi kurejesha kwa wakati.
Kasanduka ameongeza kuwa hivi karibuni amepokea barua kutoka Halmashauri inayo eleza deni la zaidi ya Milioni hamsini ambazo bado hazija rejeshwa kutoka Kata ya Ihumwa .
Kusaduka amesema kuwa Serikali haikatazi mikopo ila inaendelea kuboresha namna nzuri ya kutoa mikopo na urejeshwaji wa mikopo hiyo Ili watu wengi wanufaike na mkopo huo.
Anna Masijita Afisa maendeleo wa Kata ya Ihumwa amesema kuwa kukosekana Kwa mwendelezo wa biashara Kwa vikundi ndio sababu ya kushindwa kufanya mrejesho Kwa wakati.
Aidha Masijita ameongeza kuwa ni vema vikundi kuwa na shughuli za kufanya wanapo omba mikopo hiyo amesema vikundi vingi vinakosa sifa kutokana na kukosa biashara.