Dodoma FM

Utekelezaji ujenzi wa bomba la gesi dar es salaam hadi mombasa kukuza uchumi wa Tanzania na kenya

5 May 2021, 12:58 pm

Na; Shani Nicolaus

Makubaliano yaliyofikiwa kati ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kuhusu ujenzi wa bomba la gesi kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa yatafungua fursa za kiuchumi kwa mataifa yote mawili.

Hayo yameelezwa na Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi Enok Wiketie kutoka chuo kikuu Iringa wakati akizungumza na taswira ya habari juu ya namna Tanzania itakayonufaika na ujenzi huo ambapo amesema ajira zitapatikana kwa wingi na hata kuboresha soko la gesi nchini.

Amesema kuwa kila nchi ina ubora kiuchumi kwa nafasi yake hivo kukutana na kubadirishana mawazo kuna mambo bora na mapya yatapatikana kiuchumi na kudumisha umoja na ushirikiano.

Taswira ya habari imezungumza na wananchi jijini Dodoma ambao wamesema kuwa wanategemea  mabadiliko makubwa katika soko la Tanzania kupitia umoja huo hususani katika mazao na biashara nyingine.

Rais Samia Suluhu Hassani aliwasili nchini Kenya hapo jana katika ziara ya siku mbili ambapo amefanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Kenyatta kisha atalihutubia Bunge la nchi hiyo litakalojumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili ya nchi hiyo.