Dodoma FM

Wananchi Membe waiomba serikali kuwaboreshea huduma za afya

31 July 2023, 4:24 pm

Wazee wanasema kumekuwa na uhafifu wa huduma hali inayosababisha  baadhi yao kushindwa kumudu gharama za matibabu.Picha na Michuzi.

Sera ya afya ya mwaka 2007 inataka huduma za afya kwa wazee, wajawazito na watoto chini ya umri miaka mitano kupata huduma bure bila malipo.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa kijiji cha mlimwa kata ya Membe wameiomba serikali kuboresha huduma za afya katika zahanati yao hususani huduma za wazee pamoja na watumishi wa umma.

Miongoni mwa kundi la wazee na akinamama wamesema kumekuwa na uhafifu wa huduma hali inayosababisha  baadhi yao kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Aidha wameiomba serikali kuongeza idadi ya watumishi watakaokidhi idadi ya watu ili kupunguza changamoto  zinazoweza kujitokeza .

Sauti za wananchi wa Membe.
Wananchi hao wameiomba serikali kuongeza idadi ya wahudumu wa afya watakaokidhi wingi wa wagonjwa. Picha na Wizara ya Afya.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Musa Ngulelo amekiri kuwepo kwa ongezeko la watu ikilinganisha na wahudumu waliopo zahanati huku nao wazee wakikosa kipaumbele katika huduma.

Sauti ya Mwenyekiti.

Taswira ya habari imezungumza na diwani wa Kata ya Membe Bw.Simoni Macheho ambapo ameelezea jitihada wanazochukua kuboresha huduma za afya katika zahanati zao ikiwa ni pamoja na bima za wazee

Sauti ya Diwani