Dodoma FM

Asilimia 80 ya wagonjwa wa akili wamerithi ugonjwa huo

11 October 2023, 11:14 am

Asilimia 20 ya wagonjwa wa afya ya akili inasababisha na  mtindo wa maisha. Picha na UN news.

Inasadikiwa kuwa mtoto mmoja kati ya sita walio na umri wa chini ya miaka 18, ana uwezekano wa kuwa na tatizo la afya ya akili hata hivyo asilimia 75 ya watu hao hawapati huduma ya afya wanayohitaji.

Na Selemani Kodima.

Imeelezwa kuwa Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wa afya ya  akili wamerithi  ugonjwa huo.

Akizungumza na Taswira ya Habari mtaalamu bingwa wa saikolojia na afya ya akili kutoka Hospitali ya Afya ya Akili Mirembe, Dk Japheth Swai amesema kati ya 1 hadi  10 wenye ugonjwa wa afya ya akili nane kati yao wanakuwa wamerithi hali hiyo.

Aidha amesema asilimia 20 ya wagonjwa wa afya ya akili inasababisha na  mtindo wa maisha  .

Sauti ya Dk Japheth Swai.

Akizungumza hali ya mtindo wa Maisha kwa wazazi inavyoathiri hali ya mtoto katika familia amesema  hali hiyo inasababisha watoto kupata changamoto.

Sauti ya Dk Japheth Swai.
Asilimia 20 ya vijana kote duniani wanakabiliwa na matatizo ya akili na kujiua ambayo ni sababu ya pili kuu ya vifo. Picha na google.

Pamoja na hayo Dkt Swai amesema zipo dalili ambazo wazazi wanaweza kubaini changamoto za afya  akili ili waweze kuwafikisha kwa watalaamu wa afya ya akili ili apate msaada.

Sauti ya Dk Japheth Swai.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (Unicef) takriban asilimia 20 ya vijana kote duniani wanakabiliwa na matatizo ya akili na kujiua ambayo ni sababu ya pili kuu ya vifo miongoni mwa vijana wa umri wa kati ya miaka 15- 19 kote ulimwenguni

Akisoma hotuba ya bajeti ya Afya kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022 ilihudumia jumla ya wagonjwa 28,325 kati yao 26,761 ni wagonjwa wa akili wa nje (OPD) na wagonjwa wa akili wa ndani (IPD) 1,564.